
Rais wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, amewasilisha mpango wa kuipatia Ukraine Euro bilioni 90 kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango huo unadhamiriwa kuuwezeshaUmoja huo wa Ulaya kuwa na sauti yenye nguvu katika kuongoza majadiliano ya kutafuta amani Ukraine.
Mkopo huo kwa Ukraine kwa mujibu wa mpango uliowasilishwa, utafadhiliwa kutoka Umoja wa Ulaya au kwa fedha zitakazotokana na mali za Urusi zinazoshikiliwa katika nchi za Umoja huo. Pendekezo la kutumiwa mali za Urusi limepingwa vikali na Ubelgiji.
EU inavyopanga kutumia mali za Urusi kusaidia Ukraine
Wakati huohuo Ukraine na Urusi zimesema ziko tayari kwa mazungumzo zaidi na Marekani kuhusu kumaliza vita, baada ya kukosa kupatikana mwafaka kwenye mazungumzo yaliyofanyika jana kati ya mjumbe maalum wa Marekani, Steve Witkoff, Jared Kushner na rais Vladmir Putin.