
Lawama hizo zinatolewa ikiwa ni siku mbili kabla ya Ikulu ya Marekani kuandaa hafla ya kusaini makubaliano ya kumaliza mapigano mashariki mwa nchi hiyo. Pande zote mbili zinaumiana kwa kujaribu kuhujumu makubaliano ya amani kupitia mashambulizi katika jimbo la Kivu Kusini. Jeshi limesema wanajeshi wake walishambuliwa katika maeneo ya Kaziba, Katogota na Lubarika na kundi la waasi la M23 pamoja na washirika wake.Corneille Nangaa, kiongozi wa muungano wa waasi unaojumuisha M23, alisema kwenye ukurasa wakw wa X kwamba vikosi vya Congo, pamoja na jeshi la Burundi na washirika wengine, wameanzisha mashambulizi katika jimbo hilo.Marekani na Qatar zimekuwa zikiongoza mazungumzo yanayolenga kurejesha amani katika amjimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambako mapigano yamesababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao. Rwanda imekana kuunga mkono kundi la M23, ambalo linadai linapigana kulinda jamii za Watutsi mashariki mwa Congo.