Maafisa nchini Indonesia wanaokabiliana na hali ya mafuriko  iliyosababisha vifo vya watu 804 katika kisiwa cha Sumtra wiki hii, wameomba msaada zaidi kutoka serikali kuu ili kuondowa tatizo la ukosefu wa fedha, chakula na mafuta.

Serikali ya Indonesia  imekataa hadi sasa kutangaza mafuriko hayo kuwa janga la kitaifa licha ya kuongezeka shinikizo la kuitaka ichukue hatua hiyo. Mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa katika maeneo kadhaa ya kisiwa cha Sumtra.

Nchi hiyo imewahi kutangaza janga la kitaifa mara tatu tu katika historia yake,lilipotokea tetemeko la ardhi mnamo 1992, Tsunami mwaka 2004 na wakati wa mripuko wa Uviko 19.

Wafuatiliaji wa mambo wanasema serikali inahofia kuchukuwa uamuzi huo kutokana na wasiwasi kwamba inaweza kuwafukuza wawekezaji au  kujenga hisia za kuonekana imeshindwa kushughulikia janga hilo la mafuriko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *