Ilhan Omar, mbunge Muislamu anayewakilisha jimbo la Minnesota kwa tiketi ya chama cha Democrat amejibu mapigo kwa rais wa nchi hiyo Donald Trump baada ya kiongozi huyo kuanzisha tena mashambulizi ya matusi ya kibaguzi dhidi yake na jamii ya Wasomali wa jimbo la Minnesota.

Wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika jana Jumanne, Trump alianza tena kutoa kauli ya kibaguzi, akimwelezea Ilhan Omar na wahamiaji wengine Wasomali kuwa ni “takataka” tu na kuwataka waondoke Marekani.

“Tunaelekea kwenye njia isiyo sahihi kama tunaendelea kuingiza takataka nchini mwetu. Ilhan Omar ni takataka. Yeye ni takataka. Marafiki zake ni takataka,” alitamka bila ya aibu rais huyo wa Marekani.

Trump aliendelea kusema: “hawa si watu wanaofanya kazi. Hawa si watu wanaosema, ‘twendeni, njooni. Tupafanye mahali hapa pawe pazuri.’ Hawa ni watu ambao hawafanyi chochote isipokuwa kulalamika tu. Wanalalamika, na hawakupata chochote huko walikotoka”.

Trump ametoa tuhuma hizo dhidi ya jamii ya wahamiaji wa Kisomali katika hali ambayo, ripoti ya Chama cha Biashara cha Minnesota ya mwaka 2021 ilieleza kwamba, “japokuwa wakimbizi wengi Wasomali walifika huko wakiwa na elimu ndogo, viwango vya chini vya ushiriki wa wafanyakazi na viwango vya juu vya umaskini, hali yao miongo miwili baadaye imebadilika sana”.

Ripoti hiyo iliendelea kueleza kwamba, “viwango vya umaskini vimepungua, ushiriki wa wafanyakazi umeongezeka, mapato ya wastani ya kaya yamepanda na kiwango cha elimu pia kimeongezeka kidogo.”

Katika mjibizo aliotoa kwa matusi ya kibaguzi ya rais wa Marekani dhidi yake na jamii ya Wasomali, Ilhan Omar ameandika kwenye mtandao wa kijamii: “shauku yake isiyotulizika aliyonayo kwangu inasisimua. Natumai atapata msaada anaouhitajia mno.”

Akiwa ni mtoto mkimbizi aliyekimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia, Ilhan Omar anahesabiwa kuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuhudumu katika Bunge la Marekani. Anawakilisha wilaya ya bunge huko Minnesota ambayo ina mojawapo ya jamii kubwa zaidi za Wasomali…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *