Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)imeahirisha mkutano wa 25 wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki uliokuwa ufanyike Desemba 6, 2025 jijini Nairobi nchini Kenya.
Mshauri wa masuala ya mawasiliano ndani ya EAC, Lilian Kiarie aliithibitishia TRT Afrika taarifa za kuahirishwa kwa kikao hicho, japo hakuingia kwa undani sababu za uamuzi huo.
Hatua hiyo inakuja wakati wa uwepo wa taarifa za maandamano ya amani nchini Tanzania, yaliyoratibiwa kufanyika Desemba 9, 2025.