
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amewasili leo mchana nchini Uingereza kwa ziara rasmi ya kiserikali, akiandamana pamoja na mkewe Elke Büdenbender.
Mfalme Charles wa tatu atawakaribisha rais Steinmeier na mkewe katika kasri la Windsor mwanzoni mwa ziara yao hiyo ya siku tatu, kwa kuwaandalia mapokezi ya kifahari na sherehe ambazo kwaasili, Ufalme huo wa Uingereza huwafanyia wageni wake mashuhuri.
Ujerumani yafanya Siku ya Maombolezo
Steinmeier, ni kiongozi wa kwanza wa Ujerumani kufanya ziara rasmi ya kiserikali nchini Uingereza katika kipindi cha miaka 27.
Baadae hivi leo atakutana na waziri mkuu Keir Starmer kwa mazungumzo yatakayojikita kwenye suala la vita vya Ukraine.
Siku ya Ijumaa, rais Steinmeier na mkewe watakwenda kwenye kanisa kuu la Coventry kukumbuka mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na Manazi dhidi ya mji huo yaliyosababisha takriban, watu 568 kuuliwa,mwaka 1940.