
Rais Donald Trump siku ya Jumanne alisema hataki wahamiaji wa Kisomali nchini Marekani, akisema wakaazi wa nchi hiyo iliyoharibiwa na vita mashariki mwa Afrika wanategemea sana malipo ya serkali ya Marekani ya kujikimu na kuchangia padogo kwa Marekani.
Kuwashambulia waziwazi Wasomali walioko Marekani ni mwendelezo wa hivi karibuni wa Trump wa kuwashusha hadhi jamii nzima ya wahamiaji. Wasomali wamehamia Minnesota na majimbo mengine ya Marekani, mara nyingi kama wakimbizi, tangu miaka ya 1990. Aidha, Rais huyo hakutofautisha kati ya Wasomali wenye uraia na wasio raia.
Kauli ya Rais huyo yalikuja siku chache baada ya utawala wake kutangaza kusitisha maamuzi yote ya hifadhi kufuatia kupigwa risasi kwa wanajeshi wawili wa Walinzi wa Kitaifa huko Washington. Mshukiwa wa tukio la wiki jana anatokea Afghanistan lakini Trump ametumia muda huo kuuliza maswali kuhusu wahamiaji kutoka mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Somalia.