
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha rasimu ya azimio llinaloitaka Israeli iondoke kwenye maeneo ya Palestina iliyoyavamia na kuyakaliwa kwa mabavu tangu 1967, ikiwa ni pamoja na al-Quds Mashariki. Rasimu ya azimipia imeitaka Israel itambue haki ya watu wa Palestina ya kujitawala na kuasisi nchi huru.
Azimio hilo limeungwa mkono na nchi 151, nchi 11 hazikupiga kura. na nchi nyingine 11 zimelipinga azimio hilo.
Azimio hilo lililowasilishwa na Palestina, Jordan, Djibouti, Senegal, Qatar, na Mauritania lilipigiwa kura wakati wa kikao cha 80 cha Baraza Kuu kwa mujibu wa ajenda ya 35.
Azimio hilo linaloitaka Israel iondokea kwenye maeneo ya Palestina iliyoyakalia kwa mabavu tangu mwaka 1967 linasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa una jukumu la kudumu kuhusiana na suala la Palestina hadi litakaposhughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria za kimataifa na maazimio husika.
Azimio hilo pia limeonyesha kuwa ni muhimu kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina katikati ya mzozo wa Waarabu na Israel kupitia suluhu ya haki, ya kudumu na ya kina kwa kuhakikisha kuwa eneo la Asia Magharibi. linakuwa na amani na utulivu wa kudumu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, kanuni ya haki sawa kwa watu wote na haki yao ya kujitawala ilisisitizwa kama dhumuni na kanuni ya msingi iliyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa.
Azimio hilo lililopaishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia limeeleza kuwa Israel ambao ni utawala vamizi unapasa kujiepusha na kuwazuia Wapalestina kufuatlia haki yao ya kujitawala.