Ethiopia jana iliikosoa vikali Misri na kuituhumu nchi hiyo kwa kuyumbisha utulivu wa eneo la Pembe ya Afrika ili kudumisha ukiritimba wa kikoloni mwa Mto Nile.

Matamshi haya ya Addis Ababa yameashiria kuongezeka vita vikali vya maneno ambavyo vimeshika kasi tangu Ethiopia ilipozindua rasmi Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (Gerd), mwezi Septemba.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imedai kuwa baadhi ya maafisa wa Misri ambao wamezama katika fikra za kikoloni wanadhani kuwa wana mamlakaya kudhibiti maji ya Mto Nile. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imepinga madai ya kikoloni ya Misri sambamba na shutuma mtawalia za Cairo tangu kukamilika kwa bwawa hilo ikiwa ni pamoja na tuhuma rasmi zilizowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu kwamba Ethiopia ni tishio kuu kwa amani ya Afrika na utulivu wa kikanda.

Baada ya kuzinduliwa rasmi mwezi Septemba  Bwawa la Grand Ethiopian Renainassannce (GERD). Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri aliwasilisha rasmi malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  akitaja kuanza kazi bwawa hilo  kuwa “hatua iliyo kinyume cha sheria ya upande mmoja”; na kutahadharisha kuwa “fikra yoyote potofu kwamba Cairo itafumbia macho maslahi yake yaliyopohadaa tupu.

Ethiopia kwa upande wake inalihesabu bwawa lake hilo linalofikia thamani ya karibu  dola bilioni 5 kama ishara ya fahari ya kitaifa na muhimu kwa usambazaji wa nishati ya umeme na imekadhibisha vikali tuhuma za Misri kupitia taarifa mbalimbali.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *