Pascal Ogowé Siffon Waziri wa Utalii wa Gabon amewekwa katika kifungo cha nyumbani baada ya kukamatwa. Hatua hii imechukuliwa baada ya Waziri huyo wa Utalii wa Gabon kujaribu kuondoka Libreville.

Waziri wa Utalii wa Gabon anayetuhumiwa kwa ufisadi wa dola milioni 18 alitiwa mbaroni katika barabara kuu ya  wakati akijaribu kuondoka haraka huko Libreville, mji mkuu wa nchi hiyo. 

Siffon anashukiwa kwa ubadhirifu wa karibu dola milioni 18 zilizokusudiwa kukuza sekta ya utalii  ya Gabon. 

Wachunguzi kwa upande wao wanatarajia kuweka wazi kuhusu namna  fedha hizo zilivyotumiwa. 

Hadi sasa, hakuna uamuzi mahususi wa kimahakama ambao umetolewa, kwa kuwa suala hilo liko katika hatua ya uchunguzi.

Ingawa kumweka kitendo cha kumweka katiak kifungo cha nyumbani Waziri wa utalii wa Gabon ayetuhumiwa kwa ufisadi wa dola milioni 18  ni tukio nadra na wakati huohuo ni nyeti kwa upande wa kisiasa, lakini serikali inamhuhesabu kama shakhsia hatari sana baada ya jaribio lake la kutoroka nchi. 

Siffon, ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Utalii  Septemba mwaka 2023, tayari alikuwa amezindua miradi kadhaa ya kufufua sekta ya utalii ya Gabon. 

Miradi hiyo ni pamoja na kukagua hoteli inayomilikiwa na serikali na kuendeleza miundombinu ya utalii. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *