Kundi la madaktari wa Sudan limesema kuwa lina wasiwasi mkubwa kuhusu hatima ya makumi ya watoto na wanawake katika mji wa Babnousa huko Kordofan Magharibi, baada ya mapigano kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).

Mtandao wa Madaktari nchini Sudan umesema katika taarifa yake kuwa mapigano makali yamejiri katika  mji wa Babnousa na kwamba vitisho vinazikabili famili akatika mji huo ambazo zimepewa hifadhi katika makao makuu ya kikosi cha 22 cha jeshi la Sudan baada ya wanamgambo wa RSF kuudhibiti mji huo.

Video iliyorushwa mtandaoni na wanachama wa kikosi cha RSf zimeonyesha idadi kubwa ya wanawake na watoto wakiwa katika kambi ndani ya makao makuu hayo ya jeshi wakiwa na hali mbaya. 

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umetaka wakimbizi hao wakihakikishiwe usalama wao, wapatiwe ulinzi na kisha wahamishwe katika eneo salama bila ya kudhurika au kuweka kizuizini kiholela kwa tuhuma kwamba wana jamaa zao jeshini. 

Mtandao huo pia umetaka kuandaliwa korido salama kwa ajili ya kuwahamishia wakimbizi hao na kuwapatia misaada ya kibinadamu. 

Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeitolea wito jamii ya kimataifa kuchangia misaada na kuushinikiza uongozi wa RSF ili kuwezesha mchakato wa kuzihamisha familai zilizo karibu na maeneo yanayojiri mapigano. 

Juzi Jumanne jeshi la Sudan lilieleza kuwa vikosi vyake vimejibu mashambulizi mapya ya wanamgambo wa RSF katika mji wa Babnousa siku moja baada ya RSF kudai kuuteka mji huo na kudhibiti makao makuu ya kikosi cha 22 cha jeshi la Sudan. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *