Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani aidha Alhamisi imetoa tahadhari za usalama kwa Wamarekani wanaoishi Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba kukumbwa na ghasia zilizosababishwa na maandamano.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu, vyama vya upinzani na Umoja wa Mataifa vimesema mamia ya watu waliuawa katika vurugu hizo.

Hata hivyo, serikali imekanusha takwimu hiyo, ikisema zimeongezwa.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki na ameahidi kuchunguza vurugu hizo, baada ya machafuko hayo kusababisha mgogoro mkubwa zaidi wa kisiasa nchini humo katika miongo kadhaa.

Tanzania Arusha 2025 | Maandamano siku ya uchaguzi wa rais na wabunge
Waandamanaji waliojitokeza siku na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 nchini TanzaniaPicha: AP Photo/dpa/picture alliance

Wizara ya Mambo ya Nje imesisitiza kwamba Marekani itafanya mapitio ya kina baada ya hatua za karibuni za serikali zilizoibua wasiwasi mkubwa kuhusiana na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili lakini pia swali la ikiwa Tanzania inaweza kuendelea kuwa mshirika wa kuaminika.

“Ukandamizaji wa kidini na uhuru wa kujieleza unaoendelea kufanywa na serikali ya Tanzania, uwepo wa vizuizi endelevu kwenye uwekezaji wa Marekani pamoja na visa vya kusikitisha vya ukandamizaji dhidi ya raia katika siku za hivi karibuni na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, kwa pamoja vinatufanya kuangazia upya uhusiano wetu,” imesema wizara hiyo kwenye ya mambo ya nje.

Imeongeza kuwa hatua hizo zinawaweka hatarini raia wa Marekani wanaoishi nchini humo. Hata hivyo haikueleza ni vikwazo vipi hasa vinavyoathiri uwekezaji wake nchini humo.

Msemaji wa Tanzania Gerson Msigwa hakupatikana mara moja kuzungumzia tamko hilo la Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *