Putin ameitoa kauli hiyo katika mahojiano na kituo cha televisheni cha India Today, kabla ya kuanza ziara yake mjini New Delhi Alhamisi. Hata hivyo, kulingana na Rais huyo wa Urusi, mazungumzo hayo yalibaki kuwa ”kazi ngumu.”

Ameeleza kuwa baadhi ya mapendekezo yaliyojadiliwa hayajakubaliwa na Ikulu ya Urusi, Kremlin. Amesema mazungumzo hayo yalikuwa na vipengele ambavyo Urusi iko tayari kuvitafakari, lakini vingine havikubaliki kwa upande wa Urusi.

Ulaya yatakiwa kutokuwa kikwazo

Aidha, kiongozi huyo amezitaka nchi za Ulaya kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutafuta suluhu ya amani ya Ukraine badala ya ”kuelekea kwenye misimamo inayokwamisha.”

Matamshi ya Putin yanatolewa wakati Mjumbe Maalum wa Rais wa Marekani, Donald Trump, Steve Witkoff, pamoja na mkwe wa Trump, Jared Kushner, wanatarajiwa kukutana leo mjini Miami na kiongozi wa ujumbe wa Ukraine, Rustem Umerov, kwa mazungumzo zaidi kuhusu uwezekano wa kusaka suluhu ya mgogoro huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *