Meya wa Bat Yam katikati ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, zilizopachikwa jina bandia la Israel , amekiri kuongezeka kwa ushawishi wa kijasusi wa Iran.

Tsefika Brot ametoa tamko la dharura na kutangaza kuwa idara ya usalama wa ndani ya utawala wa Kizayuni wa Israel (Shabak) imearifu juu ya kuongezeka kwa juhudi za Iran za kupanua ushawishi wa kijasusi. Tsefika Brot ameonya kwamba “Wairani wamefika Bat Yam”; kauli inayodhihirisha nguvu ya ushawishi wa Tehran na hofu ya viongozi wa Kizayuni kuhusu kupanuka kwa ushawishi wa kijasusi wa Iran ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Meya wa Bat Yam pia alidai kuwa Shabak katika wiki zilizopita imerekodi matukio kadhaa ambapo watu wanaohusiana na Iran wamewasiliana  na raia katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, wakiwemo wanajeshi wa akiba, wanafunzi na wastaafu. Kwa mujibu wa ripoti hii, Shabak ilidai kuwa maajenti hao wa Iran walijaribu kuwavutia kwa ahadi za kifedha zenye mvuto au kwa majukumu rahisi yanayoonekana kama kusafirisha vifurushi au kukusanya taarifa.

Meya wa Bat Yam pia alifichua kuwa makumi ya wakaazi wa mji huu kwa sasa wana mahusiano ya moja kwa moja na maajenti hao wa Iran. Ripoti ya meya wa Bat Yam inaonyesha kuwa Iran imefanikiwa, kwa kutumia nyenzo rahisi lakini zenye ufanisi kama vile mawasiliano ya kifedha na  majukumu yanayoonekana kuwa yasiyo na hatari, ili kuunda mtandao wa mawasiliano ya moja kwa moja ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.

Aina hii ya kujipenyeza na kuwa na ushawishi inaonyesha ustadi wa Iran katika operesheni za kijasusi; kwa kuwa badala ya kutegemea mbinu ngumu, inatumia udhaifu wa kijamii na kiuchumi wa jamii lengwa. Mawasiliano na makundi mbalimbali kama vile wanajeshi wa akiba, wanafunzi, wastaafu,  yanaonyesha upana wa wigo wa ushawishi na uwezo wa Iran wa kuvutia watu kutoka tabaka tofauti ndani ya Israel.

Kukiri kwa viongozi wa Kizayuni kuhusu uwepo wa Iran katika moyo wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu pia kunaonyesha ubora wa kiintelijensia au kijasusi wa Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni. Uwezo huu unaweza kuipa Iran nafasi ya kupata taarifa za mapema kuhusu njama za utawala wa Kizayuni na kubuni hatua za kukabiliana nazo. Kukiri kwa meya wa Bat Yam kuhusu uhusiano wa makumi ya maajenti wanaohusishwa na Iran pia kunaonyesha mwanya mkubwa wa kiusalama katika muundo wa ndani wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).

Ushawishi wa kijasusi wa Iran, mbali na sura ya kiusalama, una pia sura ya kisaikolojia na inaashiria uwezo wa kumzuia adui. Nukta hii ni muhimu hasa kwa kuzingatia kuwa kuibua hofu miongoni mwa viongozi wa Kizayuni ni mbinu yenye nguvu na hata wakati mwingine huwa na mafanikio zaidi ya silaha za kivita.. Ushawishi wa kijasusi wa Iran ndani ya Isral si tu mafanikio ya kiutendaji bali pia ni ushindi wa kimkakati. Ushawishi huu umeuweka utawala wa Kizayuni katika nafasi ya kuchukua tahadhari ili kuepusha madara. Aidha ushawishi huu unaonyesha kuwa, licha ya madai ya Israel ya kuwa na uwezo mkubwa wa kiusalama,  utawala huu bado umebaki dhaifu mbele ya vita vya kijasusi vya Iran.

Katika vita vya siku 12 vya kichokozi vya Israel dhidi ya Iran mnamo mwezi Juni, Iran pia iliweza kwa kutumia uwezo wake wa kijasusi na kiutendaji kuushangaza utawala wa Kizayuni. Uwezo huu ulihusisha utambuzi sahihi wa malengo ya kimkakati, ambayo yalilengwa kwa makombora ya Iran, matumizi ya vita mseto, na kuibua shinikizo la kisaikolojia na kiusalama dhidi ya utawala huo.

Vita vya siku 12 vilikuwa vita vya pande nyingi na vya mseto ambapo Iran iliweza kwa wakati mmoja kutumia nyenzo za kijeshi, kijasusi, vyombo vya habari na kisaikolojia. Upana wa operesheni za Iran ulisababisha utawala wa Kizayuni kushindwa kukabiliana navyo na udhaifu wake wa kiusalama ukaonekana wazi.

Ushawishi wa kijasusi wa Iran katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu unahesabiwa kuwa ushindi wa kimkakati unaodhihirisha ubora wa nchi hii katika uwanja wa kijasusi dhidi ya utawala wa Kizayuni na washirika wake wa Magharibi.

Utawala wa Kizayuni katika miaka ya hivi karibuni daima umenufaika kwa kiwango kikubwa na msaada wa kila upande kutoka Marekani na Magharibi, lakini vita vya siku 12 na mabadiliko yaliyofuata vilifichua ukweli kwamba uwezo na ushawishi wa kijasusi wa Iran uko nje ya makadirio ya utawala haramu wa Israel  na washirika wake wa Magharibi hasa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *