Shirika la habari la Syria, SANA limeripoti kuwa ujumbe huo umewasili kupitia mpaka wa Jdeidet Yabus kati ya Lebanon na Syria, na unatarajiwa kukutana na maafisa kadhaa wa Syria na wajumbe wa asasi za kiraia.

Baada ya kuwasili ujumbe huo umelizuru eneo la Johar, Damascus ambalo limeharibiwa vibaya kwa vita.

Mkutano na Sharaa

Wanadiplomasia hao wanatarajiwa kukutana na Rais Ahmed al-Sharaa, na pia wataizuru Lebanon siku ya Ijumaa na Jumamosi.

Huku Umoja wa Mataifa ukifanya kazi kujiimarisha tena nchini Syria, Baraza la Usalama la umoja huo hivi karibuni liliondoa vikwazo dhidi ya kiongozi wa mpito Sharaa, aliyekuwa mpiganaji wa jihadi ambaye vikosi vyake viliongoza mashambulizi yaliyomuondoa Assad madarakani, Desemba 8, mwaka uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *