Mmoja kati ya miswada hiyo mitatu ulikabiliwa na upinzani kutoka kwa sehemu ya kundi la wabunge wa kihafidhina la Merz, huku tawi lake la vijana likitishia kuipinga kutokana na hofu ya gharama za baadaye kufikia mabilioni. Idadi ya wazee inayoendelea kuongezeka Ujerumani ina maana kwamba idadi iliyopo ya watu wenye umri wa kufanya kazi kuweza kudumisha viwango vya sasa vya pensheni kwa ajili ya idadi kubwa ya wastaafu inapungua. Hivyo inaongeza mzigo wa kifedha wa mfuko wa ustawi kwa kizazi kijacho.

Licha ya upinzani wa awali wa mrengo wa vijana, Merz alifanikiwa katika lengo lake la kupata kile kinachoitwa “wingi wa kura za Kansela” – kumaanisha wingi kamili wa kura kutoka kwa muungano wake wa wahafidhina na Wasocial Democrat (SPD), unaohitaji angalau kura 316 za kuunga mkono. Muswada huo ulipitishwa na kura 319 za kuunga mkono, 225 zikipinga na 53 zikisusia. Mwishowe, ni wahafidhina saba pekee waliopiga kura ya kupinga mpango huo wa mageuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *