Kombe la Dunia la 2026 ambalo ndilo gumu zaidi katika historia litafanyika Amerika Kaskazini kuanzia Juni 11 hadi Julai 19, huku timu 16 zaidi zikiongezwa kwenye mashindano hayo ya kimataifa, kutoka mataifa 32 yaliyoshiriki Qatar mwaka wa 2022.

Hafla hiyo ya Ijumaa, katika Ukumbi wa Kennedy kwenye kingo za Mto Potomac, itakuwa tukio lililojaa mastaa na watu mashuhuri lakini Trump atajiweka mstari wa mbele.

Rais wa FIFA Gianni Infantino ametengeneza uhusiano wa karibu na Trump, ikiwemo ziara kadhaa kwenye Ikulu ya White House.

Kikosikazi cha FIFA kikiwa na Rais Trump katika Ofisi ya Oval, Ikulu ya White House
Rais wa FIFA Gianni Infantino ametengeneza uhusiano wa karibu na Trump, ikiwemo ziara kadhaa Ikulu ya White HousePicha: Will Oliver – Pool via Consolidated News Photos/picture alliance

Sasa Rais huyo wa Marekani anatarajiwa kuwa mshindi wa kwanza kuwahi kupokea Tuzo ya Amani ya FIFA, ambayo itatolewa wakati wa hafla hiyo. Ni ya kutambua juhudi kubwa za watu wanaowaunganisha watu, kuleta matumaini kwa vizazi vijavyo.

Sherehe hiyo itaongozwa kwa ushirikiano na mwanamitindo Heidi Klum na mwigizaji na mchekeshaji wa Marekani Kevin Hart, na itashirikisha burudani kutoka kwa wanamuziki Andrea Bocelli na Robbie Williams.

Trump amelifanya Kombe la Dunia kuwa tukio muhimu la urais wake kwa mara ya pili na maadhimisho ya miaka 250 ya uhuru wa Marekani mwaka ujao.

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney na Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum pia watahudhuria sherehe hiyo. Viwanja kumi na moja kati ya 16 vya Kombe la Dunia viko Marekani, tatu viko Mexico na viwili vikiwa Canada.

Iran yadili msimamo

Timu ya taifa ya Iran ilifuzu kucheza Kombe la Dunia 2026
Iran awali ilikuwa imeapa kususia tukio la kupanga makundi ya Kombe la Dunia lakini baadae ikaubadili msimamo huoPicha: Sebastian Frej/IMAGO

Kipengele cha kisiasa katika droo hiyo kiliifanya Iran iape kususia tukio hilo kwa sababu Marekani ilikataa kutoa visa kwa maafisa kadhaa wa ujumbe wake.

Rais wa Shirikisho la Soka la Iran, Mehdi Taj, alilaani uamuzi huo wa Marekani akisema ni wa “kisiasa tu”. Baadaye Iran ilitangaza Jumatano kwamba sasa itatuma wawakilishi, akiwemo kocha mkuu Amir Ghalenoei. Argentina ya Lionel Messi ndiyo mabingwa watetezi baada ya kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya tatu huko Qatar mnamo 2022. Cristiano Ronaldo ataiongoza Ureno katika michuano hiyo ambayo amesema itakuwa yake ya mwisho kabla ya kutundika daluga.

Watakuwa miongoni mwa wachezaji bora pamoja na mabingwa wa Ulaya Uhispania, washindi mara tano Brazil, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza, Ureno, Uholanzi na Ubelgiji. Mataifa hayo matatu mwenyeji yanakamilisha Kundi la kwanza la timu zinazoorodheshwa juu.

Uamuzi wa kutanua mashindano pia umesafisha njia kwa mataifa kadhaa kufuzu kwa mara ya kwanza, ikiwa ni pamoja na Cape Verde, Jordan na Curacao.

Timu hizo zitagawanywa katika makundi 12 ya timu nne, huku mbili za juu kutoka kila moja zikisonga mbele pamoja na timu nane bora zitakazoshika nafasi ya tatu hadi 32 za mwisho.

Timu ya taifa ya Curacao ikishangilia kufuzu katika Kombe la Dunia baada ya kutoka sare tasa na Jamaica
Curacao, taifa dogo la kisiwa litashiriki kwa mara ya kwanza katika mashindano ya Kombe la DuniaPicha: Ricardo Makyn/AFP/Getty Images

Kwa mara ya kwanza, droo itafanyika kwa kuhakikisha mataifa manne yaliyo katika nafasi ya juu zaidi yanatenganishwa — Uhispania, Argentina, Ufaransa na Uingereza hazitaweza kukutana kabla ya nusu fainali, ikiwa zote nne zitaongoza makundi yao.

Nafasi sita kwenye mashindano hayo bado hazijaamuliwa katika mechi za mchujo, ambapo washindi watakuwa miongoni mwa timu zilizoorodheshwa chini kabisa — kwa hivyo, timu zinazopigiwa upatu zitataka kuiepuka Italia, ambayo ilishinda Kombe la Dunia hivi karibuni mwaka 2006 lakini ambayo ilishindwa kufuzu kwa mashindano mawili yaliyopita.

Mechi ya ufunguzi itachezwa katika Uwanja wa Azteca huko Mexico City, kabla ya mashindano hayo kuendelea kwa karibu wiki sita, na kumalizika kwenye fainali katika Uwanja wa MetLife nje kidogo ya Jiji la New York.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *