Serikali ya Tanzania yazidi kukabiliwa na shinikizoSerikali ya Tanzania yazidi kukabiliwa na shinikizo

Katika tamko hilo, nchi hizo zimesema zimesikitishwa na madai ya mauaji nje ya utaratibu wa sheria. Serikali ya Tanzania, hata hivyo, imeendelea kukanusha uvunjifu wowote wa sheria na kusisitiza kuwa haihitaji kuingiliwa.

Tamko hilo limeeleza masikitiko makubwa juu ya kupotea kwa watu pamoja na taarifa za kufichwa kwa miili ya waliopoteza maisha wakati wa vurugu za maandamano ya siku ya uchaguzi. Nchi hizo zimeitaka serikali ya Tanzania kuhakikisha miili ya marehemu inarejeshwa kwa familia bila kuchelewa ili ukoo na jamii waweze kufanya maziko kwa heshima.

Aidha, zimeitaka serikali kuwaachia mara moja miili ya waliouawa katika matukio ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 — hatua ambayo zinasema ni ya msingi katika kuimarisha uwajibikaji na heshima ya haki za binadamu.

Tanzania Arusha 2025 | Watu waandamana katika mitaa ya Arusha, Tanzania siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.
Watu waandamana katika mitaa ya Arusha, Tanzania siku ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.Picha: AP Photo/picture alliance

Wanadiplomasia wajadili tamko dhidi ya Tanzania

Wachambuzi wa masuala ya diplomasia wameupokea uamuzi huo kwa mtazamo mpana, wakisema Tanzania inapaswa kujitathmini upya katika namna inavyoshughulikia hatua za kiusalama na kisiasa, wakisisitiza kwamba “taifa halipo kisiwani.”

Tamko ambalo limetolewa leo linakwenda sambamba na lile la ubalozi wa Marekani lililotolewa jana, ambapo Marekani imesema inafanya tathmini mpya ya uhusiano wake na Tanzania kufuatia kile ilichoeleza kuwa ni mauaji ya raia wengi wakati wa uchaguzi huo licha ya uhusiano wa muda mrefu na wa manufaa baina ya mataifa hayo mawili.

Hotuba ya Samia baada ya kuapishwa

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

‘Wafungwa wa kisiasa waachiliwe’

Katika tamko la Umoja wa Ulaya, Uingereza na washirika wao, serikali ya Tanzania pia imetakiwa kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, pamoja na kuwapatia msaada wa kisheria na matibabu kwa wale waliokamatwa wakati wa ghasia hizo.

Hata hivyo akizungumza na wazee wa Dar es Salaam, Desemba 2 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alisema Tanzania isiingiliwe.

Mataifa mengine yaliyoshiriki kutoa tamko hilo ni pamoja na Canada, Norway, Uswisi, Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Ireland, Italia, Uholanzi, Poland, Slovakia, Hispania na Uswidi.

Kadhalika, nchi hizo zimesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa uchunguzi huru na wa wazi kuhusu matukio yote ya Oktoba 29, kwa kushirikisha asasi za kiraia, taasisi za kidini, na wadau wa kisiasakw a lengo la kuhakikisha haki, ukweli, na maridhiano vinafikiwa nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *