
Waziri wa Misaada ya Maendeleo Benjamin Dousa amewaambia waandishi wa habari kwamba Sweden itafuta misaada kwa Zimbabwe, Tanzania, Msumbiji na Liberia pamoja na Bolivia mwaka ujao na kufunga balozi zake nchini Bolivia, Liberia na Zimbabwe ambako lengo kuu lilikuwa ni misaada ya maendeleo.
Sweden inapanga kuongeza msaada kwa Ukrainehadi angalau kronor bilioni 10 za Sweden ($1.06 bilioni). Dousa amesema katika kipindi cha miaka 25 iliyopita, misaada ya Sweden kwa nchi nne za Afrika ilifikia zaidi ya kronor bilioni 50.
Waziri huyo amesisitiza kwamba mabadiliko hayo hayataathiri misaada ya kibinadamu ya Sweden, na akasema uamuzi huo unaendana na vipaumbele vya misaada vya serikali ya wachache, ambayo inaungwa mkono na chama cha Democratic cha Sweden kinachopinga uhamiaji.