Jumapili hii, Merz atakuwa mgeni wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Kansela mwenyewe amekuwa akigusia kufanya mazungumzo ya kina ya simu na Netanyahu katika kauli zake, iwe ni kuhusu hali ya jumla ya Mashariki ya Kati, mgogoro wa kibinadamu huko Gaza, au vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran. Ziara hiyo ya siku mbili inafanyika kukiwa na hoja kwamba Ujerumani inaweza kuendelea kutimiza wajibu wake wa kimataifa, kama mshiriki wa Mkataba wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kumkamata Netanyahu ambae anatafutwa na mahakama hiyo tangu Novemba 2024 kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita iwapo angeitembelea Ujerumani, kwa kuwa hilo lingehitajika kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Itakumbukwa kuwa mapemba Februari mwaka huu Merz alisema, muda mfupi kabla ya kuingia madarakani, aliamuahidi kwamba watapata mbinu za kumwezesha kutembelea Ujerumani na pia kuondoka tena bila kukamatwa katika ardhi ya taifa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *