Naibu mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ameikosoa vikali serikali ya Marekani kwa kuwawekea vikwazo majaji wa mahakama hiyo ya kimataifa, hatua ambayo amesema inaakisi jinsi Washington inavyowalenga magaidi na wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Mame Mandiaye Niang ameikosoa serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani Donald akumwambia: “Unaweza usikubaliane na kile tunachofanya lakini kamwe haupaswi kutuweke kwenye orodha ya magaidi au walanguzi wa dawa za kulevya.”

Niang, pamoja na majaji wa ngazi ya juu wa mahakama ya ICC wamewekewa vikwazo na serikali ya Trump ili kulipiza kisasi kwa mahakama hiyo ambayo imetoa waranti wa kutiwa mbaroni Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu na Waziri wa zamani wa Vita wa utawala huo, Yoav Gallant, kwa tuhuma za kuhusika na jinai za kivita na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza.  

Novemba 21, mwaka jana baada ya kuchunguza jinai za kivita na jinai  dhidi ya binadamu, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake huko Hague Uholanzi ilitoa hati za kukamatwa Netanyahu na Gallant kwa kutenda jinai ya kuwasababisha njaa kwa makusudi Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Naibu Mwendesha Mashtaka wa ICC amesema kuwa  kitendo cha kuilenga ICC, mahakama pekee ya kudumu duniani yenye jukumu la kufuatilia na kutoa hukumu kwa kesi kubwa, kinahatarisha “kuiondolea uhalali” taasisi hiyo muhimu.

Mame Mandiaye Niang ameongeza kuwa: Inatia wasiwasi kuona kwamba hati za kuwatia mbaroni Netanyahu na Gallant zimeshindwa kuwafikisha washukiwa hao mbele ya mahakama.

Image Caption

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) haina kikosi cha polisi na inategemea nchi wanachama kuwatia mbaroni washukiwa na kisha kuwasafirisha hadi mjini Hague. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *