
Maafisa kutoka nchi zote mbili wamethibitsha tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo, huku kukiwa na mvutano ulioongezeka kufuatia kushindikana kwa mazungumzo ya amani ya juma lililopita. Hakukuwa na ripoti za mara moja kuhusu vifo. Msemaji wa Taliban nchini Afghanistan, Zabihullah Mujahid, alisema kwamba wanajeshi wa Pakistan walifanya mashambulizi katika wilaya ya Spin Boldak, mkoa wa Kandahar. Kwa upande mwingine Msemaji wa Waziri Mkuu wa Pakistan aliwashutumu wanajeshi wa Afghanistan kwa “mashambulizi ya risasi bila uchokozi wowote” kandoni mwa mpaka wa Chaman. Makabiliano hayo yanafanyika ikiwa ni takribani wiki moja baada ya duru mpya ya mazungumzo ya amani kati ya majirani hao wa Asia Kusini kumalizika bila mafanikio, ingawa pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na usitishaji wao tete wa mapigano.