
Starmer atatumia mkutano na Zelensky, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz kuonyesha uungaji mkono wa Uingereza kwa Ukraine.Watajadili pia mazungumzo yanayoendelea kati ya maafisa wa Marekani na Ukraine yanayolenga kupata makubaliano ya kuhakikisha usalama wa Ukraine baada ya vita.Takribani wiki mbili zilizopita, viongozi hao wanne walishiriki katika mkutano wa mtandaoni wa kile kinachoitwa “muungano wa wenye nia” ulioitishwa na Starmer na Macron ili kutoa kikosi cha kulinda amani cha Ulaya kitakachoweza kupelekwa Ukraine iwapo kutakuwa na usitishaji wa mapigano.