Babalevo ameonyesha Mchoro wa Nyumba yake anayoijenga katika Jimbo la Kigoma Mjini na itagharimu zaidi ya Bilioni 4.
Katika ujenzi wa Nyumba hiyo inatarajiwa kutolewa ajira kwa vijana wa Kigoma Mjini 270 ambao watafanya shughuli za ujenzi wa nyumba hiyo nzuri zaidi Kigoma.
Kupitia instagram yake Mhe.Chipando ameandika;
“VIJANA 270 WATAPATA AJIRA KWENYE UJENZI WA NYUMBA NZURI ZAIDI KIGOMA …!!!
NATAKA KUHAKIKISHA ASILIMIA 70% YA BILIONI NNE ZA UJENZI ZINABAKI KIGOMA ..!!
#KILA KITU NTANUNUA KIGOMA KASORO VITU VYA DECORATION VITATOKA CHINA” Ameandika Babalevo