Jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamefanikiwa kuwakamata watu 116 kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano ya Disemba tisa.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu kamishna Wilbrod Mutafungwa amesema watu hao wamekamatwa kupitia doria maalum iliyofanyika huku akiwataka wazazi na walezi kuwaasa vijana wao kuacha kujihusisha na maandamano hayo
Katika hatua nyingine kamanda Mutafungwa amewataka waliobiwa mali zao wakati wa vurugu za Oktoba 29 na 30 kwenda kwenye vituo vya polisi kutambua na kuchukua mali zao zikiwemo injini za magari, ATM mashine za benki mbalimbali, magodoro, matenki ya maji, mitungi ya gesi pamoja na vitu vingine.