Katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, viongozi wapya wa kisiasa wameweka msisitizo katika usimamizi wa mapato, uimarishaji wa huduma kwa wananchi na kuboresha uchumi wa kaya, muda mfupi baada ya madiwani kuapishwa rasmi.
Katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, sauti mpya za uongozi zimeanza kusikika, huku Mwenyekiti mpya wa halmashauri hiyo, Edmund Rutaraka, akiahidi kuendeleza misingi ya uwajibikaji na matumizi sahihi ya fedha za umma.
Rutaraka, ambaye amechaguliwa kwa kura 23 za ndiyo kutoka kwa madiwani wote, amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha miradi inayofadhiliwa na Serikali inasimamiwa kwa viwango vya juu, ili halmashauri iendelee kupata hati safi na kuepuka hoja za ukaguzi.
Na@dixonbusagaga
#CloudsDigitalUpdates