Essam al-Din al-Sayed, mkuu wa kitengo cha utawala cha Kalogi, ameiambia AFP kwamba shambulizi hilo lililotokea siku ya Alhamisi, lilihusisha matukio matatu kwanza shambulizi dhidi ya shule ya chekechea, kisha hospitali na la tatu dhidi ya watu waliokuwa wakijaribu kuwaokoa watoto wao.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema shambulio hilo la Kordofan liliua zaidi ya watoto 10 wenye umri wa kati ya miaka mitano na saba, huku wizara ya mambo ya nje inayoungwa mkono na jeshi ikiweka idadi ya waliofariki kuwa 79, wakiwemo watoto 43.

     

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *