PLO LUMUMBA anasema, angepewa nafasi ya kuishauri Tanzania, angesema yafuatayo
👉 Angemuambia Rais aitishe mkutano wa vyama vyote vya siasa vilivyo sajiliwa Tanzania, baada hicho kikao
👉Aitishe kikao Cha asasi za kiraia zilizo hai na zilizopo kisheria.
👉Aitishe kikao cha taasisi za kidini,azungumze nao juu ya mustakabali wa Taifa.
👉Atolee majibu juu ya hoja kubwa ya watanzania na vyama vya siasa kuhusu marekebisho ya katiba, hasa kuwepo Kwa uwezekano wa kupingwa Kwa matokeo ya urais mahakamani. Tujipe muda wa miaka miwili hadi mitatu wa kufanya mapitio ya katiba na kubadili hizo Ibara, Kisha ule mwaka wa nne kuelekea wa tano uitishwe uchaguzi Sasa Kwa kuzingatia katiba mpya.
👉Awaachilie huru watu wote wenye kesi za kisiasa,
#AMANI AMANI AMANI.
Aliimba Justin kalikawe, “sisi ni watu masikini, tunahitaji kuboresha maisha, iwapo tutafanya vurugu tutashindwa kufanya kazi zetu”. Vita nyingi zilizowahi kutokea,zimekuwa zikiisha Kwa mazungumzo, kamwe vita haileti Amani, vifo vinapotokea Taifa haliwezi kutulia. Tusiruhusu vifo viendelee kutokea, Taifa litazidi kuvurugika, tutashindwa kujipatia kipato.
Watz tuliowengi, tunategemea tutoke tufanye kazi, tupate kuendesha maisha yetu, lakini Amani ikitoweka hatutaweza kufanya kazi zetu. Hasira zisiamue hatma yetu, tufikiri tunataka nini? Na je, Kwa kufanya hivi Kwa muundo na sheria za majeshi yetu tunaweza kufanikiwa Kama Kwa nguvu yetu bila support yà Jeshi hakuna kitu tunaweza kubadili, ni kwanini tusikubali maridhiano? Ok, tunasema hatuwezi kuridhiana wakati watu wamekufa, je, Kwa kufanya hivi tunaweza zirudisha Roho zilizopotea.
Tuhimize ushauri wa PLO LUMUMBA uzingatiwe. Tz irudi kuwa kisiwa Cha Amani. Mungu walinde vijana wa Tz wasipatwe na mabaya, wape mioyo ya kutambua umuhimu wa uhai wao, umuhimu wa Amani, waondolee hasira na visasi mioyoni. Amen🙏