Katika taarifa hiyo iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, Mwenyekiti wa Umoja huo wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf aliwahimiza wahusika wote wa jaribio hilo la mapinduzi kusitisha mara moja vitendo vyote visivyo halali na kurejea kwa haraka kwenye kambi zao halali na majukumu yao ya kitaalamu.

Hii leo, ubalozi wa Ufaransa mjini Cotonou uliripoti kusikika kwa milio ya risasi karibu na ikulu ya rais huku kukiwa na

ripoti zinazokinzana za jaribio la mapinduzi nchini humo.

Kundi la maafisa wa kijeshi lilichukuwa udhibiti wa televisheni ya taifa na kutangaza kwamba Rais Patrice Talon amepinduliwa.

Wanajeshi hao walisema mipaka ya nchi hiyo imefungwa na Luteni Kanali Pascal Tigri ameteuliwa kuwa rais wa “tume ya mageuzi ya kijeshi.”

Hata hivyo vyanzo vingine vya kijeshi vimesema kuwa Talon amepelekwa katika eneo salama na kwamba hali iko chini ya udhibiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *