Peskov ameiambia TASS kwamba  marekebisho ya utawala wa Trump, ambayo haiorodheshi tena Urusi kama tishio la moja kwa moja, ni  hatua chanya.

Ameongeza kuwa Urusi itaangazia kwa karibu mkakati huo uliosasishwa, na kusema unatofautiana na hatua za awali za Marekani kuelekea Urusi.

Siku ya Alhamisi, Ikulu ya White House ilichapisha mkakati mpya wa usalama na ingawa inatambua kumaliza vita nchini Ukraine kama maslahi muhimu ya Marekani, hati hiyo ina maoni machache tu ya kuikosoa Urusi.

Mkakati huo unasisitiza kuwa kumaliza uhasama ni muhimu ili kuleta utulivu wa uchumi wa Ulaya, kuzuia kuongezeka ama kupanuka kwa vita bila kukusudia na wito wa utulivu wa kimkakati na Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *