WITO WA MKUU WA MKOA WA NJOMBE RC MTAKA AKIWA KATIKA IBADA YA JUMAMOSI, KANISA LA WA ADVENTIST WASABATO NJOMBE MJINI.

1. Vijana wetu wa Kitanzania wana wajibu wa kulinda amani ya Tanzania; ninyi ndiyo kizazi kinachobeba matumaini na sura ya taifa letu.”

2. Amani ni Tunda la Haki na Wajibu,ni msingi thabiti maendeleo yetu kama jamii na kama taifa,tunao wajibu wa kuilinda Amani ya nchi yetu kwa Wivu Mkubwa,ni jukumu letu vijana wa leo,kuitunza amani yetu kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo waikute Mama Tanzania iliyo Moja.

3. Mkoa wetu bado upo salama,hauna matishio ya kihalifu,tunaendelea kujenga mazingira thabiti ya ulinzi wa watu na mali,ili kuyoa fursa kwa wananchi wetu kuendelea kufanya shughuli zao za uzalishaji mali na mahangaiko yao ya kujipatia kipato cha siku. Usalama wa mkoa wetu, utatuongezea imani kwa wawekezaji wetu mbalimbali kuendelea kuamini kwamba Njombe ni mahala sahihi pa wao kuweka mitaji yao,wana Njombe tushikamane kuhakikisha tunaziepuka aina yoyote ya chokochoko zitakazoashiria uhalibifu wa mali, uwekezaji,miradi ya umma na binafsi,au uharibifu wa uhai wa wananchi wenzetu.

4. “Wananchi Wenzangu,mkiona au kuhisi dalili yoyote hata ndogo inayoashiria uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama wa eneo lenu au maisha ya mtu,basi mtoe au utoe taarifa mapema,ulinzi shirikishi huanza na wanajamii mmoja mmoja kwa kutoa taarifa kwa wakati.” — Anthony Mtaka

Wito wangu pia kwa serikali kuna kampeni inapigwa kwa nguvu kuwa watu watoke barabarani kuwa ukiwa nyumbani ndio unakuwa katika hatari zaidi. Kuweni makini sana ni hii kauli. Pengine kuna namna inatengenezwa kutumika kudhuru watu majumbani. Hivyo ulinzi uanzie kwenye Mtaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *