“Ningependa kuwahakikishia kwamba hali imedhibitiwa kabisa na kwa hivyo nawakaribisha kuendelea na shughuli zenu kwa utulivu kuanzia jioni hii. Usalama na utulivu wa umma utadumishwa kote nchini,” amesema Rais Talon.

Rais Talon amesema hayo Jumapili jioni, baada ya mapema asubuhi kikundi cha wanajeshi kutangaza kwenye televisheni ya taifa kwamba wamempindua.

Hatua hiyo ilijibiwa mara moja na wanajeshi tiifu kwa Talon, wakishirikiana na vikosi vya Nigeria na wanajeshi kadhaa ikiwa ni pamoja na waliohusika na jaribio hilo wanashikiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *