Changamoto ya usafiri wa wagonjwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, mkoani Ruvuma, hatimaye inakwenda kufikia tamati baada ya Serikali kuleta gari jipya la kubeba wagonjwa kwa ajili ya hospitali hiyo. Kwa muda mrefu hospitali hiyo imekuwa ikitegemea magari ya halmashauri kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji rufaa au huduma za dharura.
Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wakati wa kukabidhi gari hilo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amesema serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa gari hilo, hivyo ni lazima litumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Mhe. Judith Kapinga, amesema Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi mkubwa licha ya kukosa gari la wagonjwa kwa muda mrefu. Amesema kutokana na uhitaji huo mkubwa, aliiomba Wizara ya Afya kutoa msaada huo ili kuboresha huduma za dharura na usafiri wa wagonjwa.
#CloudsDigitalUpdates