Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema, iko tayari kukabidhi silaha zake katika Ukanda wa Ghaza kwa mamlaka ya utawala ya Wapalestina itakayosimamia uendeshaji wa eneo hilo, kwa sharti kwamba uvamizi na ukaliaji ardhi kwa mabavu wa jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel ukomeshwe kikamilifu.

“Silaha zetu zinahusiana na kuwepo kwa uvamizi na uchokozi,” ameeleza katika taarifa Khalil al-Hayya, mkuu wa timu ya mazungumzo ya harakati hiyo ya ukombozi wa Palestina, ambaye pia ni kiongozi wake mkuu katika Ukanda wa Ghaza.

Al-Hayya amesisitiza kuwa: “ikiwa uvamizi utakomeshwa, silaha hizi zitawekwa chini ya mamlaka ya serikali”.

Alipoulizwa, ni serikali gani anayokusudia, mkuu huyo wa ofisi ya kisiasa ya Hamas amesema, anamaanisha nchi huru na inayojitawala ya Palestina.

Aidha Al- Hayya ameongezea kwa kusema: “tunakubali kutumwa askari wa Umoja wa Mataifa kama kikosi tofauti cha pembeni, chenye jukumu la usimamizi wa mipaka na kuhakikisha unaendana na usitishaji mapigano Ghaza”.

Wakati huohuo, mashambulizi ya anga yaliyofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel yamewaua shahidi Wapalestina saba kaskazini mwa Ghaza, akiwemo ajuza mwenye umri wa miaka 70 na mwanawe wa kiume.

Vita vya kinyama na mauaji ya kimbari yaliyoanzishwa na utawala wa kizayuni Oktoba 2023 dhidi ya Ghaza hadi sasa vimeshaua shahidi Wapalestina wasiopungua 70,354 na kuwajeruhi wengine 171,030…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *