Dhoruba kali na mvua za masika, zimepiga maeneo ya Kusini Mashariki na Kusini mwa Asiamwezi huu, na kusababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko ya ghafla, kuanzia misitu ya mvua ya kisiwa cha Sumatra Magharibi Indonesia hadi mashamba makubwa nchini Sri Lanka.

“Tunakosa kila kitu, hasa wahudumu wa afya. Hatuna madaktari,” alisema Muzakir Manaf, gavana wa jimbo la Aceh nchini Indonesia alipokuwa anazungumza na waandishi habari.

Taasisi ya kitaifa ya kushughulikia majanga (BNPB) imesema watu 961 jimboni Aceh, Sumatra ya Kaskazini na Magharibi wameuwawa kutokana na janga hilo huku 293 wakiwa hawajulikani waliko. Zaidi ya watu milioni moja wamepoteza makaazi yao.

Katika wilaya ya Pidie Jaya,  iliyoko Aceh, eneo lililoathirika vibaya na mafuriko hayo,  tembo wanne kutoka kituo cha mafunzo kilichoko karibu walisaidia kwa kuondoa vifusi vya majengo wakitumia mikonga yao na kusaidia pia kuondoa magari yaliyokuwa yamekwama huko.

Indonesien Pidie Jaya 2025 | Mafuriko yasababisha maafa makubwa Indonesia
Mvua kubwa na maporomoko ya ardhi Magharibi  mwa Indonesia yamewajeruhi watu 5,000 na kuharibu miundombinu, ikiwemo shule na hospitali. Picha: Levie Wardana/DW

Hadi Sofyan, mkuu wa taasisi ya uhifadhi wa mazingira, ameliambia shirika la habari la AFP kuwa wamewaleta tembo wanne kuondoa mabaki ya nyumba zilizosombwa na maji. Amesema nia yao ni kuondoa vifusi vyote ili wakaazi waweze kufikia maneno hayo huku akiongeza ngu tembo hao waliopewa mafunzo maalum watatumika kwa wiki nzima.

Mafuriko yaharibu miundombinu ikiwemo hospitali na shule

Mvua kubwa na maporomoko ya ardhi Magharibi  mwa Indonesia yamewajeruhi watu 5,000 na kuharibu miundombinu, ikiwemo shule na hospitali.  Katika mji wa Banda Aceh, foleni ndefu zilishuhudiwa za watu wanaotafuta msaada wa maji na mafuta  huku bei ya bidhaa nyengine kama mayai ikipanda maradufu. Taasisi ya BNPB imesema gharama ujenzi mpya baada ya janga inaweza kufikia dola bilioni 3.1.

Nchini Sri Lanka, Jeshi limepeleka maelfuya wanajeshi wake huko kusaidia katuika juhudi za uokoaji baada ya kimbunga kikali kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na kusababisha mauaji ya watu 627.

Zaidi ya watu milioni mbili ambayo ni sawa na asilimia 10 ya Idadi Jumla ya watu nchini humo wameathiriwa na Kimbunga Ditwah, kinachoelezwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kutokea kisiwani humo katika karne hii ya sasa. Sri Lanka inatarajia mvua kubwa wiki hii. Taasisi ya skuhughulikia majanga tayari imetoaoanyo kali la kuendelea kutokea kwa maporomoko ya ardhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *