Mfanyabiashara Niffer amejibu mashabiki waliomkosoa wakidai kuwa amepoteza mwelekeo na kusahau kilicho cha muhimu. Kupitia mitandao ya kijamii, Niffer amesisitiza kuwa hajawahi kuwatolea kauli yoyote ya kuwakera, bali anajaribu kuendelea na maisha yake baada ya kupitia changamoto nyingi.

Niffer amesema kuwa anaendelea kuponya majeraha yake ya kimawazo (healing her traumas) kwa kuishi maisha yake kwa utulivu bila makelele. Ameomba aachwe aishi anavyotaka bila shinikizo kutoka kwa watu.

Amesema wazi: “Am simply living my life… Nimepitia mengi mno, niache niishi maisha yangu. Naishi maisha yangu bila kelele, mtu niache please.”

Kauli hiyo imekuja baada ya baadhi ya mashabiki kumtaka asipost au kufanya jambo lolote wakihofia anaweza “kudistract” malengo yaliyopiganiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *