Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz pia watashiriki kwenye majadiliano hayo yanayolenga kuangazia namna ya kujibu mipango ya Marekani ya kuvimaliza vita nchini Ukraine.

Ziara yake inafanyika baada ya maafisa wa Ukraine kumaliza mazungumzo ya siku tatu na wenzao wa Marekani kuhusiana na mapendekezo hayo, wakati Rais wa Marekani Donald akionyesha wasiwasi ikiwa atakubaliana na pendekezo jipya la Marekani.

Ukraine na washirika wake wa Ulaya wanataka kushinikiza kwamba usitishwaji wowote wa mapigano uzingatie dhamana ya usalama kwa Ukraine pamoja na kupinga pendekezo la Ukraine kuachia maeneo yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *