
Rais Zelensky atakutana kwa mazungumzo na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na watajadili namna ya kujibu mapendekezo ya Marekani ya kukomesha vita kati ya Ukraine na Urusi.
Mazungumzo hayo yatafanyika baada ya maafisa wa Ukraine kukamilisha mazungumzo ya siku tatu na wenzao wa Marekani kuhusu pendekezo hilo huku Ikulu ya White House ikiishinikiza Kiev kuuafiki mpango huo wa amani.
Hayo yakiarifiwa, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amesema Ukraine haipaswi kulazimishwa kuachia ardhi yake kama sehemu ya makubaliano ya amani.