
Baraza la Mpito upande wa Kusini mwa nchi au STC, linaloungwa mkono na Umoja wa Falme za Kiarabu, lilidhibiti eneo la mashariki la Hadramout wiki iliyopita.
Lakini katika kile ambacho hakikutarajiwa, vikosi vinavyoungwa mkono na Saudi Arabia vilijiondoa katika eneo hilo lenye utajiri wa mafuta bila upinzani mkubwa, hii ikiwa ni kulingana na mashahidi.
Utulivu wa kiasi wa miaka ya karibuni uliibua matumaini ya amani kati ya waasi wa Houthi wanaodhibiti maeneo yenye watu wengi zaidi, kaskazini mwa taifa hilo na serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia na kutambuliwa kimataifa, iliyoko eneo la kusini.