
Wadephul amesema hayo alipozungumza na Waziri wa Biashara wa China Wang Wentao.
Wadephul amesema China ilikuwa ni mshirika muhimu zaidi wa kibiashara wa Ujerumani na kwamba Berlin inanuia kupanua ushirikiano.
Lengo kuu la ziara hiyo ni kubainisha maeneo ambayo mataifa hayo yanaweza kuimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi pamoja na kwa upande mwingine kuangazia vizuizi.
Inafanyika wiki sita baada ya Wadephul kuahirisha ziara ya awali kwa kuwa Beijing haikuwa imethibitisha mikutano na viongozi wa ngazi za juu katikati ya mvutano kuhusu Taiwan.