📶 Gharama ya 1GB Duniani: Nchi Zinazoongoza Kwa Ugali na Urahisi wa Data

Ripoti ya Cable.co.uk ya mwaka 2023 imeonesha tofauti kubwa ya bei ya 1GB ya intaneti duniani. Baadhi ya nchi zilizoendelea zinaongoza kwa kuwa na gharama kubwa zaidi, huku zingine zikiwa na gharama nafuu kupita maelezo.

🇨🇭 Switzerland inaongoza kwa bei ya juu zaidi duniani, ambapo 1GB inagharimu $7.29 ambayo ni takriban 17,950 TZS.
Nchi kama 🇺🇸 Marekani na 🇳🇿 New Zealand pia zipo juu kwa wastani wa $6.00 (≈ 14,760 TZS) na $5.89 mtawalia.

Kwa upande wa Ulaya, nchi kama 🇧🇪 Belgium, 🇸🇪 Sweden, na 🇩🇪 Germany zinauza 1GB kati ya $2.23 hadi $2.14, sawa na takriban 5,260 – 5,500 TZS.

Katika bara la Afrika, nchi kama 🇿🇦 South Africa ($1.77 ≈ 4,350 TZS) na 🇰🇪 Kenya ($0.59 ≈ 1,450 TZS) zinaendelea kuwa na bei za wastani.

Kwa upande mwingine, baadhi ya nchi zinashangaza kwa bei nafuu mno:
🇵🇰 Pakistan hutoza $0.12 (≈ 295 TZS), 🇮🇳 India na 🇮🇹 Italy zikiwa na gharama ya $0.09 (≈ 221 TZS).
Kinara wa bei rahisi duniani ni 🇮🇱 Israel, ambako 1GB ya data ni $0.02, sawa na takribani 49 TZS tu.

Takwimu hizi zinaonyesha tofauti kubwa ya upatikanaji wa intaneti duniani na jinsi mataifa yanavyotofautiana katika gharama za mawasiliano.

Kwenu GB 1 Bei Gani?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *