Jeshi la Polisi Tanzania, kupitia msemaji wake David Misime limesema kuwa mpaka mchana huu wa Disemba 9 hali ya usalama nchini ni shwari kwa maeneo yote.

Misime amesema vyombo vya ulinzi na usalama bado vinaendelea kuimarisha usalama nchini ikiwa pamoja na kulinda watu na mali zao.

Misime ameyasema hayo wakati wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya kiusalama kwa ujumla kwenye siku hii ya Disemba 9 ambapo awali kulitolewa taarifa za maandamano ya amani ambayo Jeshi la Polisi liliyapiga marufuku sababu ya kukosa kibali.

#CloudsDigitalupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *