Leo ni siku ya Uhuru wa Tanganyika (#Disemba 9) ambapo Wananchi wametakiwa kubaki majumbani kwao kama hakuna sababu ya kutoka nje ili kudumisha zaidi amani huku hali ya mitaa mingi ikiwa kimya na ulinzi umeimarishwa.
Kamera za Clouds, zimepita Bagamoyo Road kuanzia Bunju, Mbezi Beach mpaka Kawe kujionea hali ilivyo ambapo vikosi mbalimbali vya ulinzi vimeendelea kuimarisha usalama ikiwemo ukaguzi wa vyombo na abiria.
#CloudsDigitalupdates