Muungano wa Nchi za Sahel, unaoundwa na Burkina Faso, Mali na Niger, umeweka ulinzi wa anga katika hali ya tahadhari ya juu, ukiwa na mamlaka ya “kudungua” ndege yoyote inayokiuka anga yake, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa Kijeshi wa Mali, Jenerali Asimi Goita.

Waziri wa Usalama na Ulinzi wa Umma wa Mali Daoud Aly Mohamedine alipozungumzia tukio hilo amesema, “Ndege ya kijeshi ilikuwa na wafanyakazi wawili na abiria tisa ndani yake, wote wakiwa ni wanajeshi. Uchunguzi ulianzishwa mara moja na mamlaka husika ya Burkinabe na kubainika kwamba ndege hiyo haikuwa na idhini ya kuruka kwenye eneo la Burkinabe.”

Jeshi la Anga la Nigeria limesema kutua huko kulifanyika kwa mujibu wa taratibu za kiusalama za kimataifa na kwamba marubani wake wametendewa vyema na mamlaka za Burkina Faso. Ndege hiyo ilikuwa na wahudumu wawili na abiria tisa.

Tukio hili linajiri wakati uhusiano kati ya muungano wa Sahel na Nigeria ukiwa umedorora, kufuatia hatua ya Nigeria kusaidia kuzima jaribio la mapinduzi lililodumu kwa muda mfupi nchini Benin Jumapili, ambapo ndege za kijeshi za Nigeria zilifanya mashambulizi dhidi ya waasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *