Polisi imesema maandamano yamepigwa marufuku kwa kuwa mamlaka haikupokea taarifa yoyote rasmi kutoka kwa waandaaji huku kauli hiyo ikisisitizwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania George Simbachawene.

Ulinzi umeimarishwa sehemu mbalimbali hasa katika miji mikubwa kwa kuenezwa vikosi vya polisi na wanajeshi waliojihami kwa silaha. Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuondolewa kwa marufuku hiyo  na kuvitaka vyombo vya usalama kutotumia nguvu kupita kiasi katika kudhibiti maandamano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *