“Wapo wananchi ambao bado wanahofu na wapo ambao nimeona wameenda sokoni wananunua vitu vya muda mrefu kwamba labda kutakuwa na ‘lockdown’ sisi kama kamati ya amani katika mkoa wetu tunaamini bado tuko salama na wananchi wasiwe na hofu”

“Kwanza Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba hakuna maandamano lakini hata ikitokea kukawa na maandamano Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba inadhibiti maandamano hayo kwasababu si maandamano halali Serikali imeshatangaza wazi kwahiyo wananchi wawe na picha hiyo kichwani”

“Lakini tatu hatuwezi kwenda na mbinu zilezile kwa jambo lilelile wapo watu wanaotaka tuahirishe shughuli zetu za maisha sasa kwa mfano tumeambiwa tarehe 9 wataandamana na sasa hivi tumesikia tena wanasema krismasi wataandamana”

“Sasa serikali haiwezi kukaa kusikiliza watu wengine wanatupangia ratiba kwamba leo amkeni kesho fungeni shule, keshokutwa fungeni vyuo keshokutwa fungeni sheli haiwezekani”-Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda.

Cc:-Nipashe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *