Hii inafuatia mazungumzo aliyoyafanya London na Brussels Jumatatu, wakati Rais wa Marekani Donald Trump akiendelea kuishinikiza Kyiv kukubali makubaliano ya amani.

Trump amemlaumu Zelensky kwa kutosoma mapendekezo ya utawala wake, huku rasimu ya awali ikionekana kuipa Urusi faida kubwa.

Akiwa Italia, Zelensky amekutana na Papa Leo, aliyetoa wito wa amani ya haki na kudumu, kabla ya kukutana na Waziri Mkuu Georgia Meloni. Huku viongozi wa Ulaya wakiahidi “dhamana thabiti za usalama,” suala kuu limebaki kutafuta uwiano kati ya msimamo wa Ulaya na ule wa Marekani.

Zelensky amesema mpango wa awali wa vipengele 28 sasa umepunguzwa hadi 20 baada ya majadiliano ya wikiendi, ingawa amesisitiza Ukraine haiwezi kisheria wala kimaadili kukabidhi ardhi kwa Urusi.

Mpango wa Marekani unapendekeza Ukraine isalimishe maeneo ambayo Urusi bado haijayateka, badala yake ipate ahadi za usalama zisizotimiza malengo ya Kyiv ya kujiunga na NATO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *