Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, walijadiliana pia na  Zelensky kuhusu suala la kutumia mali za Urusi zilizozuiwa ili kuisaidia Kyiv kukabiliana na uvamizi wa Moscow.

Aidha Zelensky amesisitiza kuwa nchi yake haina mpango wa kuikabidhi ardhi yake kwa Urusi chini ya makubaliano yoyote ya amani na kwamba Marekani ilikuwa ikijaribu bila mafanikio kupatia mwafaka suala hilo katika mazungumzo yanayoendelea huko Florida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *