‼️‼️🔊🔊‼️‼️ Tundu A. M. Lissu alifikishwa mahakamani mara ya mwisho tarehe 12 Novemba, 2025. Tangu siku hiyo, mahakama imeshindwa kutoa ratiba mpya ya kuendelea kusikilizwa kwa kesi yake.
Kuanzia tarehe 15 Desemba 2025, likizo ya mahakama na majaji itaanza na itamalizika tarehe 31 Januari 2026.
Hadi wakati huo, Tundu Lissu atakuwa amekaa siku 80 ‼️ bila kesi yake kusikilizwa, atakuwa anaonana na kuta chakavu za gereza la Ukonga.
Mpaka kufikia januari 31, atatimiza siku 297 gerezani akiwa ametengwa na ulimwengu na chini ya ulinzi mkali unaoendelea wa saa 24/7, katika selo yake ya 6×6. Huu udhalilishaji wa utu wa mwanadamu. Hii haikubaliki. Simama na Tundu Lissu! Inuka kwa ajili yake! Na Sema kwa ajili yake.
FreeTunduLissu