Benki ya Dunia imezitahadharisha nchi maskini kuwa bado ziko hatarini huku gharama za madeni zikifikia rekodi ya juu zaidi. Benki hiyo imesema, pengo kati ya gharama za nchi maskini kulipa madeni na ufadhili mpya limefikia kiwango cha juu zaidi kwa zaidi ya miaka 50.

Benki hiyo imesema pengo hilo ni takriban dola bilioni 741 kati ya mwaka 2022 na 2024, imeshauri nchi kutumia mbinu rahisi za kifedha ili kurekebisha hali hiyo na nchi husika kupata nafuu.

Kwenye ripoti yake ya kila mwaka kuhusu madeni, benki hiyo yenye makao yake makuu mjini Washington Marekani, imesema malipo ya riba yalipanda zaidi na kuweka rekodi mpya ya dola bilioni 415.4 mwaka 2024, licha ya nafuu ndogo iliyotokana na kushushwa kwa viwango vya riba duniani.

Chanzo: DW

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *